Muonekano wa sehemu ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Dodoma sehemu ya kwanza kutoka Nala - Veyula - Mtumba - Ihumwa Dry Port (km 52.3) kwa kiwango cha lami ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 83.6, Mkoani Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde (katikati mbele) akikagua Jengo la Wizara hiyo, katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, Septemba 26, 2024.
Mwonekano wa barabara ya Mbinga - Mbamba Bay yenye urefu wa kilometa 66 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Ruvuma na kufunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 25, 2024
Muonekano wa sehemu ya barabara ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa mita 1,860 na upana wa mita 30 katika Kiwanja cha Ndege cha Songea iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Ruvuma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza taarifa kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kuhusu ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Songea mara baada ya kuwasili Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi leo Septemba 23, 2024.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour, akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ujenzi Dkt. Charles Msonde na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Eng. Mohamed Besta pamoja na viongozi wengine wakishuhudia utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi na usimamizi wa barabara ya Iringa - Msembe (km 104) kwa kiwango cha lami, Septemba 21, 2024 Mkoani Iringa.
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, akizungumza na viongozi na wananchi katika Uwanja wa Samora mara baada ya kushudia utiaji saini wa mikataba miwili ya ujeniz na usimamizi kati ya Wakala ya Barabara (TANROADS) na Mkandarasi Kampuni ya CHICO pamoja na Mhandisi Mshauri kampuni ya CIRA SAS wa barabara ya Iringa - Msembe (km 104) kwa kiwango cha lami, Septemba 21, 2024 Mkoani Iringa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta na Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya CHICO, Li Jianzheng wakionesha mkataba wa ujenzi wa barabara ya Iringa - Msembe (km 104) kwa kiwango cha lami mara baada ya kusaini mbele ya Viongozi na Wananchi, Septemba 21, 2024 Mkoani Iringa.
Kazi za ujenzi wa daraja la mto Pangani lenye urefu wa mita 525 na barabara unganishi (Km 14.3), mkoani Tanga zikiendelea. Daraja hili linajengwa na Mkanadarasi Shandong Luqiao Group.
Mhandisi Mshauri, Narayaw Bhattarai anayesimamia ujenzi wa daraja la mto Pangani lenye urefu wa mita 525 na barabara unganishi (Km 14.3) akieleza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (WaPili kulia mbele) alipokagua mradi huo, Septemba 18, 2024 mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (WaPili kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Baraka Mwambage (WaPili kulia) alipokagua ujenzi wa barabara ya Nyamwage – Utete (Km 33.7) kwa kiwango cha lami, Septemba 15, 2024 mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack (Kulia) alipokagua madaraja yaliyoathiriwa na Mvua za El-Nino zilizonyesha mwaka huu katika barabara ya Tingi- Kipatimu wilayani Kilwa, mkoani Lindi.
Mwonekano wa ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo - Busisi) lenye urefu wa Kilometa tatu linalojengwa kuunganisha barabara kuu ya Usagara - Sengerema - Geita katika Ziwa Victoria, ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 90.5, Mkoani Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo - Busisi) lenye urefu wa Kilometa tatu linalojengwa kuunganisha barabara kuu ya Usagara - Sengerema - Geita katika Ziwa Victoria, ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 90.5, Mkoani Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo - Busisi) lenye urefu wa Kilometa tatu linalojengwa kuunganisha barabara kuu ya Usagara - Sengerema - Geita katika Ziwa Victoria, ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 90.5, Mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack (Kulia) alipokagua madaraja yaliyoathiriwa na Mvua za El-Nino zilizonyesha mwaka huu katika barabara ya Tingi- Kipatimu wilayani Kilwa, mkoani Lindi.
Muonekanao wa daraja lililoathiriwa na mvua za El-Nino katika eneo la Mto Mbwemkuru lililopo mpakani mwa wilaya ya Ruangwa na Kilwa mkoani Lindi. Serikali inaendelea na hatua za ununuzi za kumpata Mkandarasi wa kujenga daraja hili.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo alipokagua eneo la Kilambo mkoani Mtwara linapotarajiwa kujengwa daraja linalounganisha Tanzania na Msumbiji kwa njia fupi, Septemba 13, 2024.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo alipokagua eneo la Kilambo mkoani Mtwara linapotarajiwa kujengwa daraja linalounganisha Tanzania na Msumbiji kwa njia fupi, Septemba 13, 2024.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo alipokagua eneo la Kilambo mkoani Mtwara linapotarajiwa kujengwa daraja linalounganisha Tanzania na Msumbiji kwa njia fupi, Septemba 13, 2024.
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akisisitiza jambo kwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Fedha ya Korea kwa ajili ya Ujenzi (K-FINCO), Dkt. Lee Eun Jae wakati alipokutana nae na kufanya mazungumzo katika jiji la Seoul – Korea Kusini, tarehe 09 Septemba 2024.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Fedha ya Korea kwa ajili ya Ujenzi (K-FINCO), Dkt. Lee Eun Jae akiwaonesha Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi (Mb), miundombinu mbalimbali ya Barabara, madaraja na majengo katika jiji la Seoul - Korea Kusini, tarehe 09 Septemba 2024.
Washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (hayupo pichani), katika Maadhimisho ya 21 ya Siku ya Wahandisi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 05, 2024.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akishuhudia Wahandisi wakila kiapo cha utii katika Maadhimisho ya 21 ya Siku ya Wahandisi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 05, 2024.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna leo tarehe 04 Septemba, 2024 Makao makuu ya NMB jijini Dar es Salaam ambapo wamejadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na fursa na uwezeshaji wa Makandarasi Wazawa pamoja na ushirikiano kati ya Benki ya NMB na Wizara ya Ujenzi kupitia taasisi zake.