Frequently Asked Questions

ATCL inatoa huduma katika Mikoa na Nchi gani?

ATCL inatoa huduma ya usafiri wa anga katika mikoa 9 . Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Mwanza, Bukoba, Kigoma, Kilimanjaro, Tabora, Dodoma, Mbeya na Zanzibar. Pia ATCL inatoa huduma katika nchi 5 ambazo ni Entebbe, Uganda; Bujumbura, Burundi; Harare, Zimbabwe, Lusaka, Zambia na Hayahaya, Comoro. Aidha, ATCL inatarajia kutoa huduma za usafiri wa anga katika miji ya Bangkok, Thailand; Mumbai,India; Johanesburg, Afrika Kusini na Guangzou, China

Temesa ina Vivuko vingapi?

TEMESA ina jumla ya vivuko 30 vinavyofanya kazi katika maeneo 20 tofauti hapa nchini. Vivuko, 26 vinafanya kazi vizuri na kivuko MV Mwanza na MV Kiu (botiyauokoaji) vimesimama kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati mkubwa.

Orodha ya vivuko ni kama ifuatavyo:

Na.

MKOA

IDADI YA VIVUKO

JINA LA KIVUKO

1.

Dar es Salaam

3

MV. Kigamboni; MV. Magogoni MV. Dar es Salaam na MV. Kazi

2.

Mwanza

11

MV. Ukara; MV. Kome II; MV. Misungwi; MV. Sabasaba; MV. Sengerema; MV. Ujenzi; MV. Nyerere; MV. Mwanza; MV.TEMESA; na MV. KIU

3

Tanga

1

MV Pangani II; MV Tanga

4

Morogoro

2

MV. Kilombero I; MV.Kilombero II

5

Kigoma

2

MV.Malagarasi; MV. Ilagala

6

Kagera

2

MV. Ruvuvu; MV. Kyanyabasa

7

Ruvuma

1

MV. Ruhuhu

8

Mara

2

MV. Musoma; MV. Mara

9

Pwani

1

MV. Utete

10

Geita

1

MV. Chato; MV. Tegemeo

11

Mtwara

2

MV. Mafanikio; MV. Kilambo