International Conference on Transport Asset Management 2025
International Conference on Transport Asset Management 2025
Muonekano wa daraja la J.P Magufuli (Kigongo Busisi) KM 3, mkoani Mwanza. Daraja hili limegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 610 na limefikia asilimia 97 kwa sasa.
Muonekano wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka, Dar es Salaam Awamu ya Nne (BRT 4) kuanzia Ubungo Daraja la Kijazi (Sam Nujoma) - Mwenge - Maktaba ya Taifa (Posta) yenye urefu wa kilometa 13.5.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akizungumza na waandishi wa habari alipofanya ziara ya kukagua miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka, Dar es Salaam Awamu ya Nne (BRT 4) kuanzia Ubungo Daraja la Kijazi (Sam Nujoma) - Mwenge - Maktaba ya Taifa (Posta) yenye urefu wa kilometa 13.5, Machi 6, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Bagamoyo (Makurunge)- Pangani-Tanga (Km 256) sehemu ya Mkange- Pangani- Tanga (Km 170.8) pamoja na Daraja la Mto Pangani (M 525) iliyofanyika wilayani Pangani mkoani Tanga tarehe 26 Februari,2025.
Muonekanao wa daraja la muda linalotumika kupitisha vifaa kwa ajili ya ujenzi sambamba na ujenzi wa nguzo za daraja la mto Pangani ukiendelea wilayani Pangani Mkoani Tanga.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo (Makurunge) - Pangani - Tanga: sehemu ya Mkange - Pangani - Tanga (km 170.8) kwa kiwango cha lami pamoja na Daraja la Mto Pangani (m 525) na barabara unganishi (Km 25) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) Februari 26,2025, mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) wakishangilia mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo (Makurunge) - Pangani - Tanga: sehemu ya Mkange - Pangani - Tanga (km 170.8) kwa kiwango cha lami pamoja na Daraja la Mto Pangani (m 525) na barabara unganishi (Km 25) Mkoani Tanga, Februari 26, 2025.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akiwa na Mawaziri wengine wakisalimiana na kufurahi Wilayani Kilindi, Mkoani Tanga katika ziara ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inayoendelea Mkoani humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Eunju Ahn katika ofisi za Wizara ya Ujenzi jijini Dodoma leo Februari 19, 2025.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Eunju Ahn katika ofisi za Wizara ya Ujenzi jijini Dodoma leo Februari 19, 2025.
Ramani ya Tanzania kuonyesha mipaka ya Utawala
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amepokea tuzo ya heshima katika mashindano ya kimataifa ya usalama wa barabara (iRAP Gary Liddle Memorial Trophy) katika mkutano wa Ten Steps to 2030 for Safer Road Infrastructure Side Event uliofanyika katika jiji la Marrakech nchini Morocco.
Mkurugenzi wa Mipango na Miundombinu wa TANROADS, Mhandisi Ephatar Mlavi akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha Miaka Minne inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO tarehe 17 Februari, 2025 jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi mara baada ya kufunga Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo , mkoani Singida, Februari 12, 2025.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza na waandishi wa habari wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea mradi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato, jijini Dodoma.
Muonekano wa Jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimatafa wa Msalato, jiini Dodoma ambalo kwa sasa limefika asilimia 51.2
Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Hakainde Hichilema akisalimiana na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega mara baada ya kuwasili nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaofanyika jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 27 hadi 28 Januari 2025.
International Seminar on Transport Asset Management
International Seminar on Transport Asset Management
Muonekano wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa jijini Dodoma ambalo ujenzi wake bado unaendelea.
Muonekano wa Daraja la Lukuledi likiendelea kujengwa Mkoani Lindi
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu (DAHRM), Bw. Mrisho Mrisho akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Mhandisi Mussa Bally Natty na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Mhandisi Rashidi Kalimbaga katika ofisi za Wizara ya Ujenzi, jijini Dodoma.
Kazi za ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga zikiendelea Mkoani Rukwa. Ujenzi wa Uwanja huo umefikia asilimia 40 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2025.